John 10

Mchungaji Mwema

1 a“Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, ni mwizi na mnyang’anyi. 2 bYeye anayeingia kwa kupitia kwenye lango ndiye mchungaji wa kondoo. 3 cMlinzi humfungulia lango na kondoo huisikia sauti yake. Huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. 4 dAkiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake. 5 eLakini kondoo hawatamfuata mgeni bali watamkimbia, kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni.” 6 fIsa alitumia mfano huu, lakini wao hawakuelewa hayo aliyokuwa akiwaambia.

7 gKwa hiyo Isa akasema nao tena akawaambia, “Amin, amin nawaambia, mimi ndimi lango la kondoo. 8 hWote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi, lakini kondoo hawakuwasikia. 9 iMimi ndimi lango, yeyote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu ataokoka, ataingia na kutoka, naye atapata malisho. 10 jMwizi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele.

11 k“Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 12 lMtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Amwonapo mbwa mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya. 13Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo.

14 m“Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua. 15 nKama vile Baba anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 oNinao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 17 pBaba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 18 qHakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”

19 rKwa maneno haya Wayahudi waligawanyika. 20 sWengi wao wakasema, “Huyu amepagawa na pepo mchafu, naye amechanganyikiwa.”

21 tWengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na pepo mchafu. Je, pepo mchafu aweza kufungua macho ya kipofu?”

Isa Akataliwa Na Wayahudi

22Wakati huo ilikuwa Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu
Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu ni Hanukkah kwa Kiebrania.
huko Yerusalemu, nao ulikuwa wakati wa majira ya baridi.
23 vNaye Isa alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Sulemani. 24 wWayahudi wakamkusanyikia wakamuuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
tuambie waziwazi.”

25 yIsa akawajibu, “Nimewaambia, lakini hamwamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yananishuhudia. 26 zLakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 27 aaKondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata, 28 abnami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu. 29 acBaba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake. 30 adMimi na Baba yangu tu umoja.”

31 aeKwa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo, 32lakini Isa akawaambia, “Nimewaonyesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni ipi katika hiyo mnataka kunipiga mawe?”

33 afWayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ingawa ni mwanadamu unajifanya kuwa Mungu.”

34 agIsa akawajibu, “Je, haikuandikwa katika Torati ya kwamba, ‘Nimesema kuwa, ninyi ni miungu?’ 35 ahKama aliwaita ‘miungu,’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka, 36 aije, mwawezaje kusema kwamba yule ambaye Baba amemweka wakfu na kumtuma ulimwenguni anakufuru, kwa sababu nilisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu?’ 37 ajIkiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msiniamini, 38 aklakini ikiwa nazifanya kazi za Mungu, hata kama hamniamini mimi ziaminini hizo kazi, ili mpate kujua na kuelewa kwamba Baba yu ndani yangu, nami ndani yake.” 39 alNdipo wakajaribu kumkamata kwa mara nyingine, lakini akaponyoka kutoka mikononi mwao.

40 amAkaenda tena ng’ambo ya Mto Yordani mpaka mahali pale ambapo Yahya alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko. 41 anWatu wengi wakamjia, nao wakawa wakisema, “Yahya hakufanya muujiza wowote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 42 aoNao wengi wakamwamini Isa huko.
Copyright information for SwhKC